MAREKANI YATOA DOLA BILIONI 30 KWA AJILI YA KULINDA MAZINGIRA, KUKUZA UHIFADHI NA UTALII


Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na balozi wa marekani Mark Childress wakisaini  mkataba wa dola Za kimarekani million 14.5 katika hotel ya Treetops Lodge ilivyo hifadhi ya wanyamapori inayosimamiwa na wananchi (WMA)  ya Randlen monduli Arusha Kwa ajili ya mradi wa kulinda mazingira, kukuza uhifadhi na utalii nchini Tanzania. (Picha na Loveness Bernard) 
Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akibadilishana mkataba na balozi wa marekani Mark Childress.


Serikali iya Marekani imetoa zaidi ya dola Bilioni 30 kwa ajili ya Kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini.

Hafla ya kutiliana saini ilifanyika jana, Seronela mkoani Arusha ambapo waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu  na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress walisaidni mmakubaliano ya dola 2milioni kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya ujangili n anyingine milioni 14.5 kwa ajili ya uhifadhi.

 Balozi huyo wa Marekani Mark Childress, alimwelezea Nyalandu, kuwa ni mwanasiasa jasiri na makini asiyeogopa kusema ukweli hata kama unaumiza.

Balozi Childress amesema waziri huyo ni tofauti na wanasiasa wengine na kwamba, ujasiri wake katika utendaji unapaswa kuungwa mkono. Kauli ya Balozi huyo imetokana na uamuzi wa Nyalandu kuweka hadharani idadi ya tembo waliopo nchini na kueleza bayana kuwa, tatizo hilo bado ni janga kwa taifa.

“Kwa mwanasiasa mwingine ingekuwa ngumu kutoa taarifa kama ile kwani angeona anajimaliza lakini alilazimika kufanya hivyo ili njia za kutokomeza tatizo hilo ipatikane na sasa marafiki wa uhifadhi tumeamua tupambane pamoja kulaliza tatizo hili”.

Pia, katika taarifa yake Nyalandu hakusita kueleza kutoweka kwa tembo 10,000 ambao hawakuweza kuonekana wakati wa sensa ya mwaka 2014 iliyofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa.

Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano na uzinduzi wa mradi mkubwa wa kulinda mazingira, kukuza uhifadhi na utalii nchini wa PROJECT, ambapo serikali ya Marekani imetoa zaidi ya sh. Bilioni 31 katika utekelezaji wa mradi huo.

Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Treetops iliyopo ndani ya eneo la Hifadhi ya Wanyamapori inayosimamiwa na jamii (WMA) kwenye Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

“Nyalandu ni mwanasiasa na kiongozi jasiri, taarifa ya sensa ya tembo ilikuwa na maeneo ambayo hayakuwa rahisi kuyasema, lakini aliamua kutangaza ili dunia ifahamu tatizo la ujangili lililopo Tanzania.

“Hii ni nadra sana kutokea kwa wanasiasa na ndio sababu Marekani imeamua kutoa msaada wa haraka katika kusaidia vita dhidi ya ujangili kwenye ushoroba wa Tarangire,” alisema Balozi Childress.

Aliongeza kuwa msaada mwingine wa haraka utatolewa kwenye maeneo mengine ya hifadhi ambayo kuna tatizo kubwa la ujangili ili kuhakikisha tembo wanakuwa salama.

Kwa upande wake, Nyalandu alisema serikali ya Rais Jakaya Kikwete, imedhamiria na imejipanga kikamilifu kuhakikisha inashinda vita dhidi ya ujangili na kwamba, itakuwa endelevu.

Alisema tatizo la ujangili bado ni kubwa licha ya mafanikio makubwa kuanza kuonekana kwa tembo kuanza kuongezeka kwenye baadhi ya hifadhi na mapori ya akiba nchini.

Aidha, alishukuru serikali ya Marekani kuendelea kuwa mshirika mkubwa wa uhifadhi na kusaidia mapambano dhidi ya ujangili nchini na kwamba, wadau zaidi hawana budi kuunga mkono jitihada hizo.

Pia, alisema serikali itaendelea kuboresha maslahi na kutoa vitendea kazi vya kutosha kwa askari wa wanyamapori nchini kwani, wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kulinda maliasili za taifa.

Alisema askari hao wamechagua kutoa maisha yao kwa uhifadhi na kulinda wanyamapori hivyo, serikali inathamini mchango huo na itaendelea kuwaboreshea maslahi na vitendea kazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.