MBUNGE WA SUMVE, NDASSA APIGANIA BEI YA PAMBA

Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndassa  akizungumza na wananchi jinsi ya kutunza lambo katika Kijiji cha Kashilili lililofunguliwa na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana Said Mwishehe, Sumve

MBUNGE jimbo la Sunve mkoani Mwanza, Richard Ndassa amemuomba Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhaman Kinana na Serikali kuhakikisha wanaangalia namna ya kuongeza bei ya zao la pamba kwani kwa sasa bei iko chini.

Ndassa alitoa kauli hiyo jana mbele ya Kinana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jimboni Sumve wilayani Kwimba mkoani hapa, ambapo alisema bei ya pamba imekwamisha maendeleo ya wananchi wa mkoa huo na hasa jimboni kwake.

Alisema wananchi wa jimbo lake wanategemea zaidi zao la pamba kama zao kuu la uchumi wao lakini kutokana na kutokuwa na bei ya kueleweka wananchi maisha yao yamekuwa magumu.

Ndassa ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 1995, alisema hata linapokuja suala la kuchangia maendeleo wananchi wanashindwa kutokana na kutokuwa na fedha kwasababu zao hilo halina bei yenye tija, hivyo ni wakati muafaka kwa Serikali ya CCM kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya zao hilo ili kuinua uchumi wa wananchi.

"Ndugu Katibu Mkuu, wananchi hawa wanajitahidi katika kilimo na eneo ambalo wanalitegemea kwa ajili ya kuimarisha uchumi wao ni zao la pamba.Kwa bahati mbaya bei iko chini, wananchi wanajitahidi kulima lakini wanaangushwa na bei.Hivyo kwenye vikao vyenu huko juu naomba mtusaidie kwenye suala la kuongeza bei ya pamba,"alisema Ndassa.

Akizungumza wananchi wa jimbo hilo,Ndassa alisema moja ya changamoto kubwa iliyopo ni uhaba wa chakula, hivyo wanaomba msaada wa chakula ili kuokoa kaya zenye tatizo la uhaba wa chakula na kutumia nafasi hiyo kuelezea kuwa tatizo hilo ni kubwa.

"Tunatatizo la uhaba wa chakula kwenye jimbo hili,hivyo tunaomba msaada wa chakula ili kunusuru maisha ya watu wetu,"alisisitiza Ndassa.

Pia alisema wananchi wanaomba Wilaya ya Kwimba kugawanywa na kupatikana wilaya mbili ya Kwimba na Sumve kwa lengo la kurahisisha maendeleo ya wananchi kwani kwa sasa wilaya ni kubwa.

Alisema wilaya hiyo itakapogawanywa wananchi wa Sumve itaweza kuwa na maendeleo makubwa na huduma muhimu zitakuwa karibu na wananchi tofauti na sasa wanalazimika kuzifuata mbali.

Ndassa akielezea huduma za afya, alisema wamefanikiwa kujenga zahanati za kutosha na jambo la kujivunia zahanati tatu zilizopo zote zina umeme wakati maeneo mengine kuna zahanati hazina umeme.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA