MCHAKAMCHAKA WA KINANA WATUA WILAYANI NGARA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuweka tone la chanjo mtoto wa miezi sita Innocent Noel  wakati wa uzinduzi wa chanjo kwa watoto katika Zahanati ya Kashinja,Kata ya Nyakisasa, wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Akihutubia baada ya uzinduzi wa chanjo hiyo, Komredi Kinana aliwataka wananchi kuachana na tabia ya kutowapeleka watoto hospitali kupata chanjo kwa sababu zisizo za masingi za kuamini mambo ya kishirikina, kwani chanjo ni kinga ya uhakika ya magonjwa mbalimbali kwa watoto. Pia katika zahanati hiyo alizindua ujenzi wa nyumba ya Mganga.
Komredi Kinana akimpatia chanjo mtoto Lillian Vicent
Ngoma ya asili ikutumbuiza wakati wa mapokezi ya Komredi Kinana, alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Benaco, wilayani Ngara leo.
Komredi Kinana akiangalia ngoma ya asili ikitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha  Benaco Kata ya Kasulo, wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera.
Ngoma ya asili ikitumbuiza katika mkutano huo wa hadhara mjini Benaco.
Komredi Kinana akisoma taarifa ya aliyopewa wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ngara.

Komredi Kinana akisaidiana na baadhi ya viongozi kumpatia fundi bati aliposhiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tawi ya CCM Munjewe, Kata ya Ruhende.
Komredi Kinana akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Francisca Katana baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kata ya Rulenge, wilayani Ngara leo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Rulenge, wilayani Ngara.
Komredi Kinana akihutubia wakat wa mkutano wa hadhara katika Mji wa Rulenge, wilayani Ngara, ambapo alisisitiza Serikali kupunguza vizuizi barabarani ili kupunguza urasmu wa kibiashara mipakani.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Komredi Kinana akisisitiza jambo hasa kuhusu suala la bei ndogo ya kahawa hapa nchini, ukilinganisha na bei ya Uganda ambayo iko juu.kitendo ambacho kinasababisha wakulima wauze Uganda ili wapate faida.
Komredi Kinana akionesha kadi mbalimbali za vyama vya NCCR-Mageuzi na Chadema alizokabidhiwa na vijana wa upinzani waliotangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa hadhara mjini Rulenge, wilayani Ngara leo.
Kadi mbalimbali za vyama vya upinzani alizokabidhiwa Komredi Kinana katika mkutano wa hadhara mjiniRulenge, wilayani Ngara.
Kwaya ikitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyikakatika Mji wa Rulenge.
Komredi Kinana akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi  kuhusu ujenzi wa Mradi wa Umeme Vijijini REA alipokwenda kukagua mradi huo uliopo Kijiji cha Djuruligwa, Kata ya Kabanga, wilayani Ngara.
Komredi Kinana akikagua Mradi wa maji Ngara mjini, unakarabatiwa kwa ghama ya sh. mil 150.
Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ngara

Komredi Kinana akihutubia mkutano wa hadhara mjini Ngara
Mmoja wa wakazi wa Ngara, akiuliza swali kwa komredi Kinana kuhusu bei kubwa ya nguzo ya umeme kitendo ambacho kinasababisha walalahoi washindwe kuingiza umeme hasa mjini.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongela akijibu maswali yaliyoulizwa na wananchi wakati wa mkutano huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.