MFUKO WA PESHNI WA PSPF WATOA ELIMU KWA MADEREVA TAXI WA WILAYA YA ILALA NA MADEREVA KUJIUNGA NA MPANGO WA HIARI


Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma akitoa maelezo ya kina kuhusu faida na huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujionga alipokuwa akiongea na madereva wa taxi wa wilaya Ilala jijini Dar 
Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai akizungumza na madereva wa taxi wa wilaya ya Ilala(Hawapo pichani) kuhusu kutii sheria za barabarani na kuwasisitiza kujiunga na mfuko wa Peisheni wa PSPF.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa azungumza jambo na madereva wa taxi wakati wa mkutano wao uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Tambaza jijini Dar
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akijibu maswali ya baadhi ya madereva 

Madereva wa Taxi wa wilaya ya Ilala wakiuliza maswali kwa Maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati wa mkutano wao
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akiwaelekeza madereva wa Taxi jinsi yakujiunga na mfuko huo
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka akimpa maelezo mmoja wa madereva wa Taxi wilaya ya Ilala aliyeamua kujiunga na mfuko wa Peisheni wa PSPF
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdalla Mohamed akimtolea ufafanuzi kuhusu faida za mfuko wa PSPF wakati wa mkutano wao uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Tambaza jijini Dar


Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka(kushoto) akimuonesha mmoja wa madereva ili aweke alama ya dole gumba kwenye fomu za Uchangiaji wa Hiari
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka akielezea jinsi ya ujazaji fomu za Uchangiaji wa Hiari kwa baadhi ya madereva waliovutiwa kujiunga na mfuko wa Peisheni wa PSPF
Baadhi ya Madreva wa Taxi wilaya ya Ilala wakiendelea kufuatilia kkwenye mkutano wao






Na Mwandishi Wetu
Madereva taxi katika wilaya ya Ilala jijini dar es salaam wapokea elimu kutoka kwa mfuko wa pensheni wa PSPF na kuweza kujiunga na mfuko huo ili kuhakikisha wanawekeza katika mfuko huo kwa manufaa yao hapo baadae kutokana na kazi zao wanazozifanya kila siku za udereva kuwa ni kazi za kawaida na kuona kuwa Pspf ndio kimbilio kwa madereva hao


Akizungumza wakati wa mkutano huo Afisa masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Ismail Juma amesema wameamua kuungana na madeeva Tax ili kuweza kuwapa elimu katika suala la kuwekeza na kufaidika na mafao mbalimbali yanayo tolewa na PSPF kwani Pindi watakapo jiunga na mfuko huo wataona matunda mengi hasa kutokana na kuwa ni watu ambao wanategemewa na familia hivyo kama Pspf wana mafao ambayo wataweza kujikwamua kama mafao ambayo wanaweza kuwasomesha watoto,vilevile fao la uzazi hata fau la nyumba pia ujiungapo na mfuko huu utafaidika na wala hauto jutia 


Mkuu wa kitengo cha elimu wa jeshi la polisi,kikosi cha usalama barabarani makao makuu , Abel Swai wakati akitoa elimu ya usalama barabarani amewaasa madereva wote nchini hususani kwa madereva walio weza kufika katika mkutano huo wa madereva tax kuweza kuwekeza katika mifuko ya jamii ni jambo muhimu hasa ukizingatia kwa hali ya sasa maisha kuwa ya kawaida na uchumi wanchi yetu kuporomoka amewaomba madereva kutumia fursa zinazo tolewa na mfuko wa pensheni wa PSPF ili wawe na akiba ya mafao yao pindi kazi zinapo isha na hata kuweza kufaidika na mambo mbalimbali katika mfuko huo


Pia mkaguzi msaidizi wa polisi kanda maalumu ya dare s salaam Josephat Sylvery Tirumanywa amewasisitiza madereva kutii sheria za barabarani maana wamepewa dhamana ya kuwasafirisha abiria kwa amani na upendo ,hivyo kati ya jeshi la polisi na madereva husaidiana kufanya kazi kwa umoja na hivyo kuweka mahusiano mazuri katika kufanikisha nchi yetu iajengwa na sisi watanzania kwa kuendeleza upendo na amani pindi tuwapo barabarani,aliongeza kuwapa shukrani mfuko wa pensheni wa Pspf kwa hatua ya kuwahamasisha watu mbalimbali kuweza kujiunga na mfuko huo ili kuhakikisha mabadiliko ya wananhi mbalimbali yanatokea kimaisha ,elimu,afya na mengine mengi.


Miongoni mwa madereva waliohudhuria katika mkutano huo wameupongeza mfuko wa pesheni wa PSPF kwa kuweza kuwajali kwa kuwapa elimu juu ya mfuko huo pia wameahidi kushiriki vilivyo katika kujiunga na mfuko huo ili kuhakikisha maisha yao yanaenda sambamba na hadhi ya jina na ubora wa kazi zinazofanywa na PSPF,
”kwani tumeiona fursa kutoka PSPF hivyo hatuna budi kujiunga na mfuko huu kwani fursa ni kuthubutu,kuhiari, kutendana kuamua na uamuzi tulio uchukua ni kujiunga na PSPF kwa manufaa ya kwetu pia ya taifa kwa ujumla “pia wawasisitiza kuendelea kueneza elimu katika mkoa wa dar es salaam wote na hata nje ya mkoa ili watu watambue fursa zinazo tolewa na PSPF.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI