MIILI YOTE 23 YA AJALI YA BASI LA ANOTHER G NA LORI MUFINDI IRINGA YATAMBULIWA , DC MBONI AWAPA USHAURI TBS KUKAGUA UBORA WA VYOMBO VYA USAFIRI


Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa Bi Mboni Mhita  kushoto  akiwa na wajumbe wa kamati ya  ulinzi na usalama wilaya hiyo ya  Mufindi  katika  kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya  wilaya ya  Mufindi
Baadhi ya  ndugu  wakichukua mwili wa ndugu  yao baada ya  kuutambua

Mkuu  wa wilaya ya  Mufindi Bi Mboni Mhita (kushoto)  akimfariji  mmoja kati ya  majeruhi wa ajali ya  basi la Another G na lori  iliyoua 23 na kujeruhi 34 jana  ,wengine pichani ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya  Mufindi (picha na matukiodaimaBlog)
 .........................................................................................................................................................


 Na MatukiodaimaBlog
MIILI yote  23  ya ajali  ya  basi  aina  Coster  mali ya kampuni ya  Another G lenye  namba  za  usajili  T 927 CEF aina ya  mitsubishi fuso iliyokuw3a ikifanya    safari  zake  kati ya Iringa – Njombe ambalo  liligoganga na   uso kwa  uso na lori  lenye namba za usajili T 916AQM  likiwa na  Tela lenye namba za usajili T 965 BEH Scania  imetambuliwa na  ndugu  zao.

Kwa  mujibu  wa  mkuu  wa wilaya ya Mufindi ambae ni  mwenyekiti wa kamati ya  ulinzi na  usalama ya  wilaya  Bi Mboni Mhita kuwa  ndugu  wa marehemu  hao  waliokufa katika ajali  waliweza  kutambua  miili ya ndugu  zao jana na leo na   kuwa hadi  sasa hakuna mwili  ambao bado kutambulia na  hivyo kuvishukuru  vyombo  vya habari kwa  kushiriki kuhabarisha  juu ya ajali  hiyo  na wananchi  ambao  waliitikia na  kufika  kutambua miili   hiyo .


Akizungumza na  mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz  leo  mkuu  huyo  wa  wilaya Bi Mboni  alisema  kuwa  jitihada  kubwa zimeonyeshwa na  vyombo  vya habari  vya ndani ya mkoa  wa Iringa na nje ya  mkoa ikiwemo mitandao ya  kijamii katika  kuhabarisha  umma na ndio  sababu ya utambuzi  wa miili  hiyo  kufanikiwa mapema baada ya habari kuenezwa vilivyo.

Pia  mkuu  huyo wa wilaya   alipongeza  uongozi  wa JKT Mafinga   na uongozi  wa kitaifa  wa jeshi   hilo kwa  kujitolea  kusaidia mazishi  ya  vijana wake  ambao walikuwa wakielekea JKT Mafinga kwa ajili ya  kuripoti kwa kuanza mafunzo ya jeshi na   baadhi yao  kufa katika ajali  hiyo  huku baadhi  wakijeruhiwa kwani alisema ni  vigumu kwa taasisi  kujitolea  kusaidia mtu ambae hana mkataba  nae.

Aidha  mkuu  huyo  wa  wilaya aliwaomba  wananchi wote  nchini ambao ndugu  zao walipoteza maisha katika ajali ya basi la Majinja lililoua  watu  zaidi ya 50 katika  eneo la Changalawe  mjini Mafinga  kufika kituo  cha  polisi Mafinga kwa ajili ya kutambua  na kuchukua mizigo ya  ndugu  zao  waliopoteza maisha katika ajali hiyo na kuwa mali  zote za marehemu hao zimehifadhiwa salama.
Hata  hivyo  mkuu  huyo  wa  wilaya ya  Mufindi Bi Mboni alivitaka  vyombo  vya   usalama  barabarani katika  wilaya ya Mufindi  kuendelea na mkakati  wake wa  kuwabana madereva wanaovunja  sheria  za  barabarani na kuwachukulia hatu kali kama  njia ya  kupunguza ajali  hiyo.

Alisema askari  hao  pia  wanapaswa  kukagua ubora  wa  vyombo  vya usafiri vyote na  vile ambavyo havina  ubora  ni heri  kuvifungia  hadi vitakapoboreshwa  kuliko  kuruhusu vyombo  vya  usafiri  chakavu  kufanya kazi  ya usafirishaji  wa abiria .

Kuhusiana na wajibu  wa  shirika la viwango Tanzania (TBS) mkuu  huyo wa wilaya  alishauri kuwepo na mkakati makini wa TBS  kukagua  ubora  wa vyombo  vya usafiri vinavyoingizwa  nchini kwani mabasi  mengi ya abiria  siti   zake zimeshikiliwa na ngundi ya mbao na baada ya kutokea ajali siti hizo  hung'oka na kama abiria amefunga mkanda hulazimika kuchomoka na siti yake .

Alisema katika ripoti ya ajali ya kwanza ya basi la Majinja  iliyotokea Machi  mwaka huu na kuua watu zaidi ya 50   kamati ya uchunguzi  ilibaini hilo na  kuwa  mwenye uwezo wa  kukagua  viwango  vya vyombo  hivyo  vya usafiri ni TBS kwa kushirikiana na wadau wengine kama Sumatra   na jeshi la polisi  kupitia kitengo  cha usalama barabarani.

Wakati  serikali ya  wilaya ya  Mufindi kupitia mkuu  huyo wa  wilaya ikishauri TBS na  washirika  wake  kuweka mkakati wa kukagua   viwango  vya vyombo   hivyo  vya usafiri baadhi ya  wananchi   wilaya ya  Mufindi na mkoa wa Iringa wamekuwa na maoni  tofauti kwa  kulitaka jeshi la polisi kitendo  cha askari wa usalama barabarani kuanza kusindikiza mabasi hayo yanayotoka  usiku mkoani Njombe na Iringa ili  kuhakikisha abiria   hawazidi katika mabasi hayo ya usiku.

Zacharia Sanga  mkazi  wa Mafinga  wilaya ya Mufindi na John Lumwesa mkazi  wa Iringa mjini  walisema kuwa  kimsingi mabasi hayo  yanajaza  abiria  kupita  kiasi na kutembea kwa mwendo mkali  zaidi kutokana na nyakati za usiku  askari  wa usalama barabara  kutokuwepo.

Hivyo walitaka  askari  wa usalama barabarani  kuendelea kuwepo na tochi hadi usiku ili  kuthibiti ajali mbaya kama  hiyo ambayo mbali ya  kuwa ni uzembe wa dereva  wa basi ila kukosekana kwa askari  wa usalama barabarani  usiku ni  moja ya  sababu.

Mganga  mkuu  wa  Hospitali  ya  wilaya ya  Mufindi Dr  Godluck  Mlimbila  alisema  kuwa hali za majeruhi 34 waliokuwa  wamelazwa katika  Hospitali   hiyo zinaendelea  vizuri na  kuwa mbali ya  wale  wanne ambao  hali  zao  zilikuwa mbaya  zaidi na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya   mkoa wa Iringa katika Hospitali  hiyo hadi jana majira ya saa 8 mchana  ni majeruhi kati ya 8 na 10  pekee  ndio ambao  walikuwa  wakiendelea na matibabu   huku  wengi  wao wakiwa  wameruhusiwa baada ya hali  zao  kuendelea  vema .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU