Mwenge wa uhuru wazindua miradi ya Bilioni 1.2 Mufindi ,kiongozi wa mbio za mwenge asifu serikali ya awamu ya nne ataka wananchi kuchagua viongozi bora


Picha: mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita(kushoto) akikabidhiwa Mwenge na mkuu wa Wilaya ya Iringa Angelina Mabula jana mwenge huu umezindua miradi 13 yenye thamani ya zaidi ya Tsh bilioni 1.2( picha na Francis Godwin)

JUMLA ya miradi 13 yenye thamani ya zaidi ya Tsh bilioni 1,290,654,123 imezinduliwa na mbio za mwenge wa Uhuru wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Akitoa taarifa ya miradi hiyo jana mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Bw Juma Chum , mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita alisema kuwa katika miradi hiyo wananchi wa Mufindi wamechangia kiasi cha zaidi ya Tsh 831.6 huku wahisani wakichangia kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 172.3

Pia alisema kwa upande wa serikali kuu imechangia jumla ya kiasi cha zaidi ya Tsh 134.6 na halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imechangia Tsh milioni 151,985,908.

Mkuu huyo wa Wilaya aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa vyumba 3 vya maabara Kinyanambo sekondari,jengo la Saccos wanawake (Faraja Saccos),ujenzi wa barabara km 14.4 Mtili hadi Mkuta,ujenzi wa zahanati na Nyumba ya mganga kijiji cha Mtili .

Miradi mingine ni pamoja na mradi wa Hifadhi ya mazingira Mtili,klabu ya kupambana na rushwa Itedero sekondari,mradi wa Trecka kwa wakulima kijiji cha Lugolofu,ujenzi wa Josho kijiji cha Lugolofu,mradi wa kopa ng'ombe lipa Ng'ombe kijiji cha Lugolofu,ujenzi wa ofisi ya kijiji Mabaoni,ujenzi wa ofisi ya kata Makungu na mradi wa maji Mgololo

Hata hivyo mkuu huyo wa Wilaya pamoja na kuwashukuru wahisani mbali mbali kwa jitihada zao za kuchangia miradi hiyo ya maendeleo bado aliwapongeza wananchi wa Mufindi kwa kuendelea kuhamasika kuchangia miradi hiyo na kuwataka kuwapuuza baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ambao wanapinga wananchi kuchangia mwenge.

Alisema kuwa mbio za mwenge wa uhuru pamoja na kutumika kuwaunganisha watanzania pia mbio hizo za mwenge wa uhuru ni chachu kuwa ya kuhamasisha maendeleo na kutolea mfano miradi hiyo ambayo imetekelezwa kwa kipindi kifupi zaidi.

Kwa upande wake kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kitaifa Bw Chum mbali ya kuwapongeza wananchi hao wa Mufindi kwa kuwa na miradi mizuri ya kimaendeleo bado alisema wananchi hawanabudi kutumia vema haki Yao katika uchaguzi mkuu kwa kuchagua viongozi wapenda maendeleo badala ya kuchagua viongozi wapinga maendeleo.

Alisema muda wa uchaguzi ukifika wananchi wote wanapaswa kwenda kushiriki kuchagua viongozi makini zaidi na kupongeza jitihada kubwa za serikali ya awamu ya nne chini Rais Dr Jakaya Kikwete.

Hivyo alisema iwapo wananchi watachagua viongozi bora wapenda maendeleo nchi itasonga mbele zaidi katika maendeleo ya elimu,Afya ,miundo mbinu na miradi mingine mingi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.