UCHAGUZI WA RAIS NA WABUNGE BURUNDI WAAHIRISH



Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.SERIKALI ya Burundi imetangaza kuwa uchaguzi wa Rais na Wabunge uliotarajiwa kufanyika mwezi huu umeahirishwa mpaka tarehe nyingine zitakazotangazwa.
Vurugu Burundi.Msemaji wa Rais Nkurunziza, Wily Nyamitwe amesema kuwa tarehe hizo zitapangwa na wasimamizi wa uchaguzi wa nchi hiyo hivi karibuni.
Mabadiliko hayo yamekuja kutokana na taifa hilo kuingia kwenye machafuko tangu Rais Piere Nkurunziza kutangaza nia ya kuongoza kwa awamu ya tatu.
Umoja wa Mataifa umeelezea jinsi mgogoro huo ulivyoongeza idadi ya wakimbizi wanaoikimbia Burundi, hivyo kumtaka rais huyo kuachia ngazi mwezi huu kama makubaliano ya Azimio la Arusha yalivyoelekeza.
Uchaguzi wa wabunge ulitarajiwa kufanyika kesho Ijumaa (Juni 5) na wa urais ulipangwa Juni 26, mwaka huu.
CREDIT: BBC

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU