WAZIRI MEMBE AWASIHI WATANZANIA KUTOCHAGUA VIONGOZI WANAOSAKA UONGOZI KWA KUTOA RUSHWA


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe akimkabidhi Bi. Shamim Khan tuzo ya heshima ya kujishughulisha na kazi za kijamii hapa Tanzania,katika tamasha la kwanza la Qaswida
lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania. PICHA NA MICHUZI JR.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Sheikh Ismail Mohamed wakati wa tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulamaa Qaswida Promotions ambao ndio waandaji wa tamasha la kwanza la Qaswida,Ustaadh Jumanne Ligopora akimkaribisha mgeni rasmi  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Mh.Bernard Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe  akizungumza katika tamasha hilo la kwanza Qaswida, lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa,Mh Membe amewataka Watanzania kusubiri kwa hamu siku ya kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,

Alisema siku hiyo ya Juni 6, wananchi wasikilize nini anataka kuifanya nchi iweze kuondoka ilipo ikiwemo kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo. “Mkae tayari siku hiyo, naamini uongozi mzuri wa nchi ni ule wa kudumisha amani na utulivu na ili nchi iweze kusonga mbele, maadili kwa viongozi ni muhimu,” alisema Waziri Membe.

Membe alitumia nafasi hiyo kuwasihi Watanzania kuacha kuchagua viongozi ambao kwa nje, wanajinadi  wana dini, lakini matendo hayaendani na maadili ya  dini zao. Alisema ili mtu aweze kuaminika kuwa ana dini, jamii ifuatilie katika madhehebu yao, hivyo amewasihi wasichague viongozi wanaosaka uongozi kwa kutoa rushwa.

“Msikubali kuwa na viongozi ambao kwa nje, wanaojinadi kuwa na dini kinyume na matendo yao, lazima mchague wenye hofu ya Mungu ambayo husisitizwa na dini zote,” Alisema uongozi wa heshima ni ule unaochukia rushwa ambayo ni adui wa haki, hivyo amewataka wananchi kuwaogopa wapenda rushwa kama ukoma. 
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria tamasha hilo.
Baadhi ya Washiriki waliofika kwenye tamasha hilo la kwanza la Qaswida.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.