Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Kata ya Masumbwe, akiwa
katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika
wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Juni 17, 2015.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa Katibu Mkuu
wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika katika kata ya Masumbwe, wilayani
Mbogwe mkoani Geita.
Katibu w NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo, wakati wa mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Mbogwe akisalimia wananchi
Katibu w NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo, wakati wa mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Mbogwe akisalimia wananchi
Wananchi
wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdlrahman Kinana alipohutubia maelfu
ya watu katika mkutano wa hadhara uliofanya katik kata ya Masumbwe,
utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe
mkoani Geita.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati ya Kata
ya Kashelo, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya
ya Mbogwe mkoani Geita.
Wananchi
wa Kata ya Kshelo, wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, baada ya kukagua
na kushiriki ujenzi wa zahanati yao, utekelezaji wa ilani ya CCM na
uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwapokea wanachama wapya wa CCM,
waliohama kutoka Chadema, katika mkutano wa hadhara aliofanya katika
Kijiji cha Lugunga, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika
wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na kijanaAugustine Gerald
na kuahidi kumpeleka Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), alipokagua ujenzi wa
nyumba ya Mwalimu katika Kijiji cha Lugunga, utekelezaji wa ilani ya
CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimsikiliza kwa makini, Diwani wa
Nyakafulwa, Mathias Nyororo, aliyekuwa akifafanua kutoanza kwa mradi wa
maji kijiji cha Masumwe, licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa fedha za
mradi huo miezi sita iliyopita. Iikuwa ni baada ya wananchi kulalamika
kutopata maji katika kijiji hicho katika mkutano wa hadhara ambao Kinana
aliufanya katika kata ya Masumbwe, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai
wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivuka kwenye daraja duni, wakati
akienda kukagua mradi wa ujenzi wa shule katika kijiji cha Lyamchele,
utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Bukombe
mkoani Geita, jana, Juni 16, 2015. Tayari serikali imeanza mpango wa
ujenzi wa daraja imara katika Kijiji hicho.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisafirishwa kwa pikipiki, baada ya
kuvuka daraja duni kwenda kijiji cha Lyamchele kukagua ujenzi wa shule,
utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe
mkoani Geita.
Wananchi
wa Kijiji cha Lyamchele, wakiwasindikiza kwa ngoma na Kisukuma, Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye, baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule katika kijiji hicho.
Vijana wanaojishughulisha na kutafuta madini ktika udongo wa masalia, wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).
Comments