Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na
mwandishi wa habari wa Gazeti la Main Post la Mjini Wurzburg Nchini
Ujerumani baada ya kulitembelea jingo la Serikali linalotumika kwa kwa
shuhuli mbali mbali ikiwemo shuhuli za Utalii rais na ujumbe wake
alitembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kikazi.
[Picha zote na Ramadhan Othman,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein
wakipata maelezo kutoka kwa Mario Gerth (kulia) wakati waalipotembelea
katika kituo cha maonesho ya picha Spitale katika Mji wa Wurzburg picha
hizo zenye kuonesha Zanzibar na Ustaarabu wa Waswahili zilizotayarishwa
chini ya nusimamizi wa Dr.Stefan Oschman Mkurugenzi wa Tamasha la Muziki
wa Afrika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mratibu na
Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Zanzibar Amber Resort Bi Naila Jidawi wakati
alipotembelea mabanda ya maonesho ya Kazi na sanaa za Mzanzibar katika
viwanja vya maonesho katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa
katika ziara ya kikazi nchini humo juzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein
wakipata maelezo kutoka kwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Nd,Issa Mlingoti wakati
alipotembelea mabanda ya maonesho ya Kazi na sanaa za Mzanzibar katika
viwanja vya maonesho 27 ya Muziki wa Afrika katika Mji wa Wurzburg
Nchini Ujerumani akiwa katika ziara ya kikazi nchini na ujumbe nwake
juzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein
wakiangalia picha za ramani ya ujenzi wa Mradi wa Zanzibar Amber Resort
Bi Naila Jidawi wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Kazi na
sanaa za Mzanzibar katika viwanja vya maonesho katika Mji wa Wurzburg
Nchini Ujerumani akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo juzi.
Katibu
Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Nd,Saleh Ramadhan Feruzi
alipokuwa akitoa maelezo kwa wageni wakitalii mbali mbalio waliofika
katika mabanda ya kazi mbali mbali kutoka Zanzibar wakati wa Maonesho ya
Tamasha la 27 ya Muziki wa Afrika yaliyomalizika juzi katika viwanja
vya Wurzburg Nchini Ujerumani ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
alipofanya ziara ya kikazi ya siku nane nchini humo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein
wakiangalia kazi mbali mbali za kiutamaduni wa Zanzibar ikiwemo kusuka
ukili,mikoba na utiaji wa hina na wanja kwa watalii waliotembelea
mabanda ya maonesho ya Kazi hizo katika viwanja vya maonesho katika Mji
wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo
juzi.
Mchoraji wa mauwa kutumia wanja na hina
akiwaremba watalii wakati wa maonesho ya 27 ya Tamasha la muziki wa
Taarab kutoka Zanzibar pia Tamasha lilijumuisha wasanii mbali mbali wa
fani hiyo kutoka nchi mbali mbali Duniani na kazi za kiutamaduni katika
kuitangaza Zanzibar Kiutalii katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani
juzi,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mkewe Mama
Mwanamwema Shein (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Nd,Saleh Ramadhan Feruzi walipoangalia
kazi mbali mbali za uchoraji ikiwa ni katika hatua za kukuza Utalii wa
Zanzibar katika mabanda ya maonesho ya Kazi hizo katika viwanja vya
maonesho katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa katika ziara ya
kikazi nchini humo juzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein
(kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Masoko Salum A.Kibe wakati walipoangalia
bidhaa mbali mbali za karafuu ikiwa ni katika hatua za kukuza Utalii
wa Zanzibar katika mabanda ya maonesho katika Mji wa Wurzburg Nchini
Ujerumani juzi akiwa katika ziara ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akibadilishana mawazo
na Viongozi wa baada ya kutembelea sehemu mbali mbali za maonesho ya
Tamasha la 27 la Muziki ambapo Zanzibar ilishiriki kujitangaza
kiutalii na kuonesha bidhaa mbali mbali katika maonesho hayo
yaliyofanyika katika viwanja vya Eneo maalum lililotengwa Mjini Wurzburg
Nchini Ujerumani katika ziara ya kiazi ya siku nane nchini humo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake walipofika
katika viwanja vya maonesho na kuwatembelea wasanii wa kikundi cha
muziki wa Taarab cha Matona kutoka Zanzibar na kuwapa moyo katika
jitihada zao za kuitangaza Zanzibar Kiutalii Nchini Ujerumani katika
Tamasha 27 la Muziki katika ziara ya kiazi ya siku nane nchini humo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein
wakifuatana na Dr.Stefan Oschman Mkurugenzi wa Tamasha la Muziki wa
Afrika baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Zanzibar katika Mji wa
Wurzburg Nchini Ujerumani katika hatua zakuitangaza Zanzibar kiutalii.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiagana na Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Tropiki Prof.Dr.med.Augustin
Stich baada ya Taasisi ya Tafiti mbali mbali yakiwemo magonjwa ya
Binadamu, Chuo cha Afya katika Mji wa Wurzburg kimeweza kutoa mchango
mkubwa katikakupambana na maradhi ya Ebola yaliyotokea Nchi za
Magharibi,
Comments