HABARI MPASUKOOOOO MBOWE AZUNGUMZIA KUPOTEA KWA DK SLAA


Akizungumza na Radio one mda wa saa 4, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe, amesema Dr Slaa hawezi kuhama chama hicho na hafikirii kamwe, kwa sasa anapumzika kwa likizo ya wiki moja. 

Alipoulizwa kuhusu Slaa kutokubaliana na ujio Wa Lowassa amejibu kila kitu tulikubaliana na Slaa mwenyewe aliunga mkono suala hilo.
Mbowe amesema wananchi na wanachadema kwa ujumla wasiwe na wasiwasi kwani hiki chama ni makini na hakiwezi fanya maamuzi bila maridhiano na akasisitiza kuwapuuza wanaoeneza habari kuwa Slaa amejiuzulu siasa.
Alipoulizwa mara ya mwisho kuwasiliana na Dr Slaa ni lini akajibu jana saa kumi na mbili jioni.
Alipoulizwa walizungumza nini akajibu anajua yeye na Slaa.
Walipomuuliza hasa mbona sisi tukimpigia hapatikani akajibu sijui lakini mimi nimewasiliana nae jana.


Chanzo: Radio one

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*