Chalila Kibuda,Globu ya jamii
UGONJWA wa kipindupindu unazidi kusambaa katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi habari leo Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,Aziz Msuya
watu waliofariki katika manispaa hiyo watatu.
Amesema idadi ya wagonjwa katika manispaa imezidi kuongezeka kutoka 34 hadi kufikia 43.
Amesema
dalili za huo ni homa kali ,kuharisha pamoja na kutapika na kuongeza
kuwa mtu akifikia dalili hizo awahi katika kituo cha afya.
Aidha amesema kujiepusha na ugonjwa huo ni kuzingatia usafi wa vyakula ,maji pamoja na kunawa mikono kwa usafi wakati wa kula.
Msuya amesema watu waliokuwa wamelalazwa na ugonjwa huo watatu wamerusiwa.
Katika zahanati ya Mburahati wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa ni 21.
Muuguzi Mkuu wa Zahanati hiyo, Nusra Kessy amesema kuwa wagonjwa hao wanaendelea kutibiwa katika zahanati hiyo.
Usafi ukiendelea katika Zahanati ya Mburahati katika kukabiliana na
Ugonjwa Kipindupindu mara baada ya Globu ya Jamii kutembelea kujionea
hali halisi ya ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
Wakati
ugonjwa wa kipindupindu ukiwa umeshika kasi lakini watu bado wanakula
holela kama walivyokutwa na Kamera yetu leo jijini Dar es Salaam.
Usafi
wa Mazingira katika Zahanati ya Mburahati ukiendelea kama walivyokuwa
na Globu ya Jamii leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel
Massaka,Globu ya Jamii)
Comments