Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema
kuwa uamuzi wa Sekta Binafsi kukubali kubanwa na sheria, taratibu na maadili ya
kukabiliana na rushwa ni hatua kubwa ya kubadilisha mapambano (Game Changer)
dhidi ya rushwa nchini.
“Hapa
sasa tunaongeza utamu kwenye keki (icing on the cake) kwa sababu hii ni mara ya
kwanza katika historia ya nchi yetu kwa sekta binafsi kukubali kubanwa na
maadili ya mapambano dhidi ya rushwa,” Rais Kikwete amesema leo, Ijumaa, Agosti
14,2015 wakati alipozungumza katika Halfa ya Uzinduzi wa Ahadi ya Uadilifu.
Katika
hafla hiyo iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amekuwa kiongozi wa
kwanza nchini kutia saini Hatia ya Ahadi ya Uadilifu ambayo itatiwa saini na
viongozi wote wa umma, watumishi wote wa umma na viongozi wa sekta binafsi
nchini ikiwa ni hatua nyingine za kuzidi kupambana na rushwa na kuboresha
utawala bora nchini.
Rais
Kikwete amewaambia viongozi waliohudhuria hafla hiyo kuwa viongozi wa umma
nchini wamekuwa na miiko, tarartibu na kanuni mbali mbali ambazo zimekuwa
zinawabana na kuongoza maadili yao tokea uhuru wa Tanzania. “Hawa wamekuwa na
nyaraka nyingi ambazo zimekuwa zinawabana tokea uhuru wa nchi yetu. Lakini
sekta binafsi haijapata kuwa na miiko ya namna hii.”
Rais
Kikwete ameongeza kusema kuwa hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa sekta binafsi
kukubali kubanwa na miiko ya uongozi na katika hafla ya leo, Sekta Binafsi
imewakilishwa na Mwenyekiti wa Watendaji Wakuu wa Makampuni nchini, Ndugu Ali
Mufuruki ambaye pia ni Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Infotech
Investments.
Ndugu
Mufuruki pia ametia saini Hati ya Ahadi ya Uadilifu kwa niaba ya Sekta Binafsi
nchini.
Rais
Kikwete pia ametoa changamoto kwa sekta binafsi, akiwataka watendaji wa sekta
hiyo kujitokeza na kutoa habari kuhusu rushwa kwa sababu kwa kuwa baadhi ya
watendaji na watumishi wa sekta bianafsi ni washiriki katika rushwa kwa maana
ya kuwarubuni watumishi wa umma na viongozi wa sekta ya umma.
Amesema
kuwa ni jambo lisilokuwa na manufaa kwa watendaji wa sekta binafsi kukaa tu na
kulalamika kuwa kuna rushwa nchini wakati wao pia ni washiriki.
“Jitokezeni
waziwazi na kutupa habari ya watu ambao wanawadai rushwa walioko katika sekta
ya umma. Kujitolea habari za namna hii kutasaidia. Na katika hili mtu haihitaji
wala kushindwa na sharia yoyote. Ni wajibu wake kama raia bora.
Ahadi
ya Uadilifu ni moja ya hatua ambazo zilipendekezwa na wadau katika moja ya
warsha za kujadili jinsi gani ya kukabiliana na balaa la rushwa nchini chini ya
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao ulianzishwa na Serikali ya Rais
Kikwete.
Wadau
hao walitoa pendekezo hilo kwa Serikali kama moja ya njia za kuzidi
kukabilaiana na rushwa nchini.
Ends
Comments