Picha ya marehemu James Bukumbi ikiwa mbele ya waumini wakati wa ibada leo.
Watoto wa marehemu mzee Bukumbi,
Eric Shigongo (wa kwanza kulia), Marsha Bukumbi (wa kwanza kushoto) na
baadhi ya ndugu wakiweka shada la maua katika kaburi la baba yao.
Eric Shigongo akielezea historia
ya baba yake, marehemu James Bukumbi wakati wa ibada ya kumbukumbu ya
miaka mitatu tangu kifo chake.
Padri George Nzungu ambaye ni
Paroko wa Parokia ya Mt. Kizito, Kabila, Magu akiongoza ibada ya
kumbukumbu ya miaka mitatu ya mzee Bukumbi.
Wanafamilia ya James Bukumbi wakiwa katika ibada hiyo ya kumbukumbu.
Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika ibada ya kumbukumbu ya miaka mitatu ya mzee Bukumbi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Global Publishers, Eric Shigongo ambaye ni mmoja wa watoto wa mzee
Bukumbi akitoa sadaka wakati wa ibada hiyo.
Mmoja wa wakurugenzi wa Global Publishers, Marsha Bukumbi ambaye pia ni mtoto wa marehemu akishiriki ibada ya kumbukumbu.
Lydia Bukumbi ambaye naye ni mmoja wa wakurugenzi wa Global Publishers naye akitoa sadaka yake wakati wa ibada ya leo.
Mhariri wa Gazeti la Championi Jumamosi, Elius Kambili naye kitoa sadaka yake wakati wa ibada ya leo.
Wanakwaya wakiimba wakati wa ibada hiyo.
Padri George Nzungu (kulia) akisaidiana na Padri Ibrahimu Ngassa kuongoza ibada hiyo.
Ibada ikiendelea nyumbani kwa marehemu mzee James Bukumbi.
Safari ya kuelekea makaburini.
Wanafamilia wakiwa katika kaburi la mzee Bukumbi.
Ibada ikiendelea katika kaburi la mzee Bukumbi.
Wanafamilia wakiwa na shada la maua wakati wa ibada ya kumuombea mzee Bukumbi.
Mapadri wakiweka shada la maua katika kaburi la mzee Bukumbi wakati wa ibada hiyo.
Masista nao wakiweka shada la maua.
Diwani wa Kata ya Bupandwamhela,
Masumbuko Machimwi (wa kwanza kulia) na Diwani wa Kata ya Katwe Kanyumi
Henry (wa pili kulia) wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mzee
Bukumbi.
Baadhi ya wajukuu wa kike wa mzee Bukumbi wakiweka shada la maua kwenye kaburi la babu yao.
Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers wakiweka shada la maua katika kaburi la mzee Bukumbi.
KUMBUKUMBU ya miaka mitatu tangu
kufariki kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Publishers &
Gen. Enterprises Ltd, James Bukumbi imefanyika leo katika kijiji cha
Bupandwamhela, wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Ndugu, jamaa na marafiki
wameungana na familia ya marehemu James Bukumbi katika ibada ya misa ya
kumbukumbu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Bupandwamhela.
Ibada hiyo ya kumbukumbu
imeongozwa na Padri George Nzungu ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mt.
Kizito, Kabila, Magu akisaidiana na Padri Ibrahimu Ngassa.
Katika mafundisho yake, Padri
Nzungu amewaasa waumini kumuweka Mungu mbele katika maisha yao ya kila
siku na kutenda matendo mema huku akitumia muda mwingi kuwafariji
wanafamilia, ndugu, jamaa na wanakijiji waliohudhuria kuwa marehemu
James Bukumbi yuko mahali salama na wazidi kumuombea.
(PICHA: DENIS MTIMA, BRIGHTON MASALU NA IDD MUMBA / GPL, BUPANDWAMHELA)
Comments