Maalim SEIF SHARIF HAMAD akutana na Wagombea wa CUF – Pemba

Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad, akizungumza na viongozi pamoja na wagombea wa chama hicho katika
ukumbi wa skuli ya Fidel Castro Kisiwani Pemba.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad, akisalimiana na mgombea uwakilishi wa CUF Jimbo la Ole baada ya
kutambulishwa kwa wagombea rasmi wa Ubunge na Uwakilishi.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar
Ismail Jussa Ladhu, akizungumza na viongozi pamoja na wagombea wa chama hicho katika
ukumbi wa skuli ya Fidel Castro Kisiwani Pemba.
Na: Hassan Hamad (OMKR)
Chama Cha Wananchi
CUF kimesema kimejipanga vyema ili kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinapata
taarifa za kuwaeleza wananchi kuhusiana na chama hicho kuanzia ngazi za
majimbo.
Katibu Mkuu wa Chama
hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kupitia timu za ushindi wa chama
hicho kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu ujao, chama hicho kitatoa taarifa
kwa vyombo vya habari katika ngazi zote kuanzia ngazi ya majimbo, Wilaya hadi
Taifa.
Amesema lengo la hatua
hiyo ni kuondosha urasimu wa upatikanaji wa habari ndani ya chama hicho, ili
kuwawezesha wananchi kupata taarifa zinazokwenda na wakati kupitia vyombo vya
habari vya ndani na nje ya nchi.
Maalim Seif ameeleza
hayo katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro kisiwani Pemba, wakati akizungumza
na viongozi pamoja na wagombea wa chama hicho kwa majimbo 18 ya Pemba.
Amefahamisha kuwa kwa
mujibu wa taratibu zilizowekwa na chama hicho, kamati tendaji za Taifa, Wilaya
na Majimbo sasa zinageuka kuwa timu za ushindi, na kuwataka wajumbe wa kamati
hizo kufanya kazi kwa mashirikiano ili kuhakikisha kuwa wanakipatia ushindi
mkubwa chama hicho.
Amefafanua kuwa Chama
hicho hakitokuwa na muhali kwa mtendaji yeyote atakayekiuka maadili ya Chama,
na kuwaagiza viongozi wa Wilaya na Majimbo  kuwa makini na kuwawajibisha watendaji watakao
zembea.
Wakati huo huo Kaimu
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Ismail Jussa Ladhu amesema wakati chama hicho
kikijiandaa kuchukua fomu za uteuzi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar, hakitotoa barua kwa mgombea yeyote aliyeshindwa kulipa
madeni yake ndani ya chama hicho.
Amesema Chama hicho
hakitokuwa na muhali na jambo hilo, na iwapo mgombea atashindwa kulipa madeni
hayo, Kamati tendaji Taifa inaweza kuteua mgombea mwengine wakati wowote.
Ameeleza kuwa hatua
hiyo inalenga kudumisha nidhamu ndani ya chama hicho na kuwafanya wanachama
kuwa na imani na viongozi wao.
Chama
hicho tayari kimetangaza timu yake ya kampeni kwa upande wa Zanzibar inayoongozwa
na Naibu Katibu Mkuu Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akisaidiwa na Mansoor Yussuf
Himid, ambapo kwa upande wa Pemba kampeni za Urais wa Zanzibar kupitia Chama
hicho zitaratibiwa na Mjumbe wa Kamati Tendaji Taifa Mhe. Hamad Massoud Hamad
akisaidiwa na Waziri wa Habari Mhe. Said Ali Mbarouk.
Aidha
chama hicho cha CUF kimekabidhi seti 40 za jezi na mipira 120 kwa kila jimbo
kati ya majimbo 18 ya Pemba na kukamilisha utaratibu wake wa kutoa vifaa kama
hivyo kwa majimbo yote 54 ya Zanzibar.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI