Mkurugenzi
wa Msama Promotions akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ofisi za
kampuni hiyo,jijini Dar kuhusiana na kuandaa tamasha la kuiombea
Tanzania inayoelekea kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika,Oktoba
25 mwaka huu,Tamasha hilo linatarajia kufanyika Oktoba 4.
KAMPUNI
ya Msama Promotions imeandaa Tamasha kubwa la kihistoria ambalo
halijawahi kufanyika nchini la kuiombea Tanzania inayoelekea katika
uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Alex Msama Tamasha hilo litafanyika Oktoba 4, jijini Dar es Salaam.
Msama
alisema kutokana na uzito na heshima ya tamasha hilo, linatarajia
kushirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili wa ndani na nje ya
nchi ambao wanaotamba katika tasnia ya muziki huo.
Alisema
japo ni mara ya kwanza kwa kampuni yake kuandaa tamasha kama hilo
katika historia ya uchaguzi nchini, anaamini kwa vile amani ni kitu
muhimu katika uchaguzi, wengi watamuunga mkono.
Msama
alisema anaamini wengi watajitokeza kuungana pamoja na viongozi wa
kitaifa na kada mbalimbali kuuombea uchaguzi huo ambao ni njia ya
kidemokrasia ya kupata viongozi kwa ngazi ya urais, ubunge na udiwani.
“Watanzania
wajiandae kuiombea amani Tanzania kupitia muziki wa Injili hasa
waimbaji mbalimbali wa kutoka nje ya Tanzania watashiriki katika tukio
hilo ambalo bado tuko katika mchakato wa mahali tutakapofanyia,” alisema
Msama na kuongeza:
“Tamasha
hilo kubwa kimaudhui linakaribia Tamasha kubwa la Pasaka ambalo
hufanyika kila mwaka tangu mwaka 2000,” alisema Msama aliyechangia kwa
kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili.
Aidha
Msama alisema baada ya tamasha hilo kufanyika jijini Dar es Salaam,
watahamishia maombi hayo katika majiji mengine manne kwa lengo hilo la
kuombea amani na utulivu uchaguzi Mkuu.
Alitaja nchi watakazotoka waimbaji watakaosindikiza maombi hayo niAfrika Kusini, Rwanda, Kenya, Uganda, Zambia, Burundi na DR Congo.
Comments