WAGONJWA 100 WA UGONJWA WA MABUSHA KUFANYIWA UPASUAJI MANISPAA YA MTWARA

X4
Kaimu Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa kambi hiyo ya upasuaji Johansen Bukweri akizungumza kwenye uzinduzi huo, alisema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yamekuwa yakiathiri sehemu kubwa ya jamii katika mkoa wa Mtwara na kuleta mahangaiko mengi kwa wananchi ikiwemo ulemavu, hali ambayo inapunguza uwezo wa wananchi kushiriki katika ujenzi wa Taifa na watoto kutoweza kuhudhuria vizuri katika masomo shuleni
X1
Mratibu wa Taifa wa Mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira, akielezea majukumu ya mpango huo wakati wa uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye tatizo la ugonjwa wa mabusha Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara,iliyofanyika katika hospitali  ya Mkoa ya Ligula.
X2
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) na Mwenyekiti wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele Afrika Dkt. Mwele Malecela akitoa salamu kwenye uzinduzi wa kambi hiyo, ambapo alisema Matende na mabusha ni magonjwa ambayo yanatakiwa kutokomezwa ifikapo mwaka 2020 nchini Tanzania.
X3 
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ,wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibimayila, akipokea mfano wa hundi toka kwa mwakilishi wa Stat Oil Naomi Makota (kulia) kwa ajili ya upasuaji wa wagonjwa wapatao 100 wa Manispaa ya Mtwara.
X5
Kaimu Mkuu wa Wilaya akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye ugonjwa wa mabusha.
X6
Dkt. Upendo Mwingira akiwafariji wagonjwa waliokwishafanyiwa upasuaji wa mabusha katika hospitali ya mkoa ya Ligula.Upasuaji huo ni wa siku 5.Mkoa wa Mtwara una takribani watu wapatao 2,500 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa mabusha.Kambi hii itafanyika kwa watu waliojiandikisha na itatolewa bila ya malipo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*