WATU 7 WA FRAMILIA MOJA LINDI WAFARIKI DUNIA KWA MATUKIO TOFAUTI


Familia ya Jacky Magongo ambayo ni maarufu sana hapa Lindi mjini ilitikiswa na majaribu mazito ya misiba ya ndugu 7 wa familia hiyo ndani ya siku 3 tu. 
Mnamo tarehe 2/8/2015 bwana Shiraz ambaye ni Mtoto mkubwa wa mzee Jack anayeishi Nachingwea alikuwa Lindi mjni na gari yake binafsi ili kumpokea binti mkubwa wa dada ake aliyetokea Dar .
Ili aweze kwenda naye Nachingwea mara atakapomaliza taratibu za kusalimiana na jamaa zao wa hapa Lindi mjini.
Baadae walianza safari ya nachingwea wakiwa kwenye gari iliyowabeba watu wa nne yaani bwana shirazi, mpwa wake, mjukuu wake na dereva, kwa bahati mbaya walipata ajali kabla hawajafika Nachingwea.
Katika ajali hiyo bwana shirazi na binti yake huyo walikufa hapohapo, lakini dereva na mtoto wa yule binyi walijeruhiwa vibaya sana na kukimbizwa hospitali. 
Mnamo taerehe 3/08/2015 miili ya marehemu ililetwa Lindi mjini na kufanyiwa taratibu za mazishi, baada ya kumaliza kuzika tarehe 4/08/2015.
Wakapata taarifa kuwa nyumba ya dada yao (mama wa yule binti aliyefariki kwenye ajali ya kuelekea Nachingwea) iliyopo Dar 
Ilikuwa inaungua moto na kulikuwa na mtoto ndani ya nyumba hiyo, hivyo kwa haraka sana ikambidi dada huyo amchukue mama yao mzazi pamoja na wajukuu zake wawli ili warudi Dar haraka.

Lakini kwa bahati mbaya wakiwa katika kijiji cha Mavuji gari yao aina ya noah iligongana uso kwa uso na gari nyingine na wote wanne pamoja na dereva kupoteza uhai hapohapo.

Wakati wakijiandaa kushughulikia hilo zikaja taarifa kuwa yule kijana aliyekuwa hoi baada ya ajali ya tarehe 3 naye amefariki pamoja na mtoto aliyekuwa kwenye nyumba inayoteketea kwa moto.

Mungu azilaze mahala pema peponi roho za marehemu hawa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI