Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akipokewa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Capt. Mstaafu Aseri
Msangi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kwa ziara
ya siku mbili mkoani humo tarehe 2.10.2015. Aliyesimama kushoto ni
Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akishiriki kucheza ngoma ya utamaduni na wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga
kilichoko katika wilaya yaTarime kwa ajili ya kuzindua rasmi Shule ya
Sekondari ya J. K. Nyerere iliyojengwa na Kampuni ya Acacia inayomiliki
Mgodi wa North Mara Gold Mine tarehe 2.10.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akijumuika na viongozi wa Mkoa wa Mara na wanachi wa Kijiji cha Myamwaga
kusherehekea uzinduzi rasmi wa Shule ya J.K. Nyerere iliyojengwa na
North Mara Gold Mine.
Mke wan a Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mkuu wa
Wilaya ya Tarime Ndugu Glorius Luoga muda mfupi baada ya kuwasili
kwenye Kijiji cha Nyamwaga kwa ajili ya uzinduzi wa Shule ya Sekondari J
K Nyerere.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akitoa hotua ya uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari J.K.Nyerere katika
Kijiji cha Myamwaga kilichoko Mkoani Mara.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akishirikiana na viongozi wa Mkoa wa Mara na wale wa Wilaya ya Tarime
na wahisani waliojenga Shule ya J.K. Nyerere kukata utepe ikiwa ni
ishara ya uzinduzi rasmi wa Shule hiyo iliyoko katika Kijiji cha
Nyamwaga.
Comments