MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF) KIGOMA WAWAKUMBUKA WAZEE LEO KATIKA SIKU YAO.

Baadhi ya wafanyakazi wa mfuko wa bima ya afya NHIF kigoma wakikabidhi msaada wa vyakula kwa uongozi wa kituo cha Silabu cha kulelea wazee wasiojiweza ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
 Meneja wa Mfuko wa bima NHIF  ya kigoma akisalimiana na wazee wanaotunzwa katika kambi ya Silabu kata ya kibirizi
Baadhi ya wazee wasiojiweza wanaoishi na kutunzwa katika kambi ya kulea wazee ya Silabu kata ya Kibirizi Mkoani hapa.
 Na Editha Karlo.Kigoma
MFUKO wa Bima ya afya (NHIF)wametoa msaada wa  vyakula kwa wazee wasiojiweza uliopo katika kituo cha silabu kata ya kibirizi mjini hapa.
Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo wa chakula Meneja wa Mkoa wa mfuko huo Elius Odhiambo alisema kuwa mfuko unatumbua umuhimu na mchango wa wazee kwa jamii.
"Sisi kama mfuko wa bima ya afya tuna thamini sana na kutambua mchango wenu wazee kwa jamii kwani kila mmoja wetu ni mzee mtarajiwa"alisema odhiambo
Alisema wamekabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi milioni moja na elfu sitini,vyakula walivyotoa ni mchele kilo 100,sukari kilo 100,unga wa ugali kilo 100,maharage kilo 100 na mafuta ya kupikia kilo 20
Meneja huyo alisema wataendelea kusaidiana na kuwasaidia wazee hao kila inapobidi.
Naye mkuu wa kituo hicho cha kutunzia wazee Juma Ndikamukana wasiojiweza aliushukuru mfuko wa bima ya afya kwa msaada wao huo na kuwakumbuka wazee katika siku yao leo.
Alisema kituo hicho kina jumla ya wazee 51 wasiojiweza wanaotunzwa wanaotoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA