MIKUTANO YA MWAKA YA KUNDI LA BENKI YA DUNIA NA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA YAANZA RASMI NCHINI LIMA
Dr. Servacius
Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali wa
katikati akiwa pamoja na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu kushoto
na Bi. Natujwa Mwamba Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania kulia, wakiwa katika
mkutano wa chombo kinachotoa mafunzo ya kusimamia mambo ya uchumi (MEFMI)
nchini Peru – Lima. ( Picha na Eva Valerian, Peru – Lima).
Mikutano
ya mwaka ya Bodi ya Magavana ya Shirika la fedha la Kimataifa na kundi la Benki
ya Dunia kwa mwaka 2015 imeanza rasmi hapa mjini Lima –Peru na kuhudhuriwa na maelfu
ya watu kutoka nchi mbalimbali Duniani ambapo kilele chake kitakuwa tarehe 12 mwezi
Octoba 2015.
Bodi
ya Magavana wa Shirika la Fedha la kimataifa ( Mfuko) na Bodi ya Magavana wa kundi
la Benki ( Benki ) kwa kawaida hukutana mara moja kwa mwaka kujadili kazi za Taasisi
ambazo ziko chini yao. Mikutano hii ya mwaka huwa inafanyika mwishoni mwa mwezi
Septemba na mwanzoni mwa mwezi Octoba. Mikutano hii hufanyika mjini Washington
kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama
ambaye amepitishwa kutokanana na viwango
vilivyowekwa.
Mikutano
hii ya Bodi ya Magavana ilizinduliwa huko Savannah, Georgia, Amerika mwaka 1946
na ikaanza kufanyika mjini Washington DC mwaka huo huo.
Mikutano
hii ya mwaka itaambatana pamoja na mikutano ya kimataifa ya kifedha, kamati za
fedha, Kamati za maendeleo, kundi la nchi kumi, kundi la nchi ishirini na nne,
na makundi mbalimbali ya nchi wanachama.
Aidha
katika kuhitimisha mikutano hii, Shirika la fedha la kimataifa, kamati ya mambo
ya fedha, Kamati ya maendeleo pamoja na makundi mengine watapata nafasi ya kuwasiliana
na kutoa mapendekezo yao ya kipi kifanyike ili kuhakikisha mambo wanayojipangia
yanatekelezwa.
Magavana
watakitumia kipindi hiki kwa kuzungumzia
masuala ya kibiashara na kushauriana.
Bodi ya Magavana inatumia kipindi hiki
kufanya maamuzi ya ni vipi mambo ya Fedha ya kimataifa yanapaswa kuwa na
kukubaliana kuhusu maazimio yao.
Comments