MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AFANYA MKUTANO NA AKINA MAMA ZAIDI YA 300 KUPAMBA NA KIPINDUPINDU SHINYANGA
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa mkutano
wake na wanawake zaidi ya 300 katika manispaa ya Shinyanga uliofanyika
katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine
alisema wanawake ni jeshi kubwa na ni walimu wakubwa katika familia
hivyo wana nafasi kubwa ya kupambana na kipindu pindu kwa kuimarisha na
kuhamasisha usafi kwa akina baba,watoto na hata wanawake wenzao.
"Kipindu
pindu ni hatari sana...kinaua lazima tupambane nao kwa nguvu
zote..nimewaita ili kila mmoja ajue Shinyanga tuna janga..sasa kila mtu
achukue hatua,ugonjwa huu unatokana na uchafu..akina mama mna nafasi
kubwa sana katika hili...."alisema Matiro.
Hapa ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako wanawake/akina mama zaidi ya 300 wa manispaa ya Shinyanga wamekutana kujadili namna ya kupambana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umeukumba mkoa wa Shinyanga.Mkutano huo umeitishwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Akina mama hao waliojitokeza kwa wingi leo jioni Oktoba 06,2015 wameweka mikakati mbalimbali ya kutokemeza ugonjwa kipindupindu ambapo Jana pekee wagonjwa 9 wamelazwa katika kambi maalum jirani na hospital ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambapo kati ya hao 9 wawili wamefariki dunia.
Comments