Mmoja
wa wafanyakazi wa Chama Cha Albino, Christina Mbedi akielezea namna
Chama cha Albino kinavyofanya kazi zake kwa Meneja wa Chapa na
Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale wakati wa ziara ya viongozi wa
Zantel ofisini kwao. Anayetizama kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Umoja
wa Albino Tanzania, Ernest Kimaya.
Meneja
wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale akikabidhi msaada wa
vifaa vya mawasiliano kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Albino
Tanzabua, Ernest Kimaya. Wanaotazama nyuma ni baadhi ya viongozi wa
Chama cha Albino.
Meneja
wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale akikabidhi msaada wa
vifaa vya mawasiliano kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Albino
Tanzania, Ernest Kimaya. Anayetazama nyuma ni mmoja wa viongozi wa Chama
cha Albino.
Viongozi wa Chama cha Albino na Zantel wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya Viongozi wa Zantel kutembelea ofisi zao.
- Yaiunganisha ofisi ya chama cha albino na huduma ya mtandao pamoja na mawasiliano ya simu
Dar
es Salaam, 8/10/2015:
Uongozi wa Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo umetembelea ofisi za Chama
cha Maalbino Tanzania, ziara yenye lengo la kujifunza zaidi kuhusu Chama cha
Maalbino kinavyofanya kazi pamoja na kuboresha ushirikiano baina yao.
Pamoja na kuzungumza na viongozi wa
chama cha Maalbino, uongozi wa Zantel pia umekabidhi huduma za simu, kwa kuwapa
namba maalumu pamoja na kuwaunganisha na huduma ya mtandao.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo,
Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Progress Chissenga alisema huu ni mwendelezo wa
ushirikiano baina ya Zantel na Chama Cha Maalbino.
‘Leo tumeamua kuja kuwatembelea
wenzetu wa Chama cha Maalbino ili kujionea namna wanavyofanya kazi, na msaada
huu wa intaneti pamoja na huduma ya simu tuliyokabidhi leo itawawezesha
viongozi na watendaji wa chama cha albino kupiga simu bure kwa mwaka mzima,
lakini pia itarahisisha mawasiliano baina yao na viongozi wengine wa chama
kutoka mikoani’ alisema Chissenga.
Katika ziara hiyo, viongozi wa Zantel
na Chama cha Maalbino Tanzania walijadiliana maeneo mengine ya kuongeza
ushirikiano baina yao katika kuhakikisha chama cha Maalbino kinatekeleza
majukumu yake zaidi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama
cha Albino Tanzania, Bwana Ernest Kimaya, alisema wanaishukuru kampuni ya
Zantel kwa kuendelea kuwaunga mkono katika juhudi zao za kuhakikisha mauaji ya
albino yanamalizika nchini.
‘Tunawashukuru Zantel kwa kuendelea
kutuunga mkono na msaada huu waliotukabidhi leo, unaonyesha kuwa wana nia ya
dhati ya kushirikiana na chama chetu’ alisema Kimaya.
Ziara
hii ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya Kampuni
ya simu za mikononi ya Zantel na Chama cha Maalbino Tanzania, ambao ulilenga kusambaza
elimu juu ya ulemavu.
Comments