ZUNGU-SOGEZENI HUDUMA ZA MAWASILIANO KWA WANANCHI

MBUNGE wa jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam,Mussa Hasan Zungu  ameyaasa makampuni yanayotoa huduma za simu nchini kuzidi kuzidi kubuni huduma za kurahisisha  maisha kwa wateja na kusogeza huduma zaidi kwa wananchi ili wazipate popote walipo.

Zungu aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa duka jipya linalotoa huduma mbalimbali za Vodacom lililopo barabara ya uhuru Kariakoo katika mwendelezo wa kampuni hiyo kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo  imefungua maduka katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini. “Nawapongeza kwa kusogeza huduma hasa katika kipindi hiki ambacho sekta ya mawasiliano inazidi kukua siku hadi siku”alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema kuwa kampuni imejipanga kuendelea kuboresha huduma zake na kuwekeza zaidi katika kuimarisha huduma  ili kuwawezesha wananchi na wateja kwa ujumla kuzipata kwa urahisi.

“Sisi kama kampuni tunaamini kuwa tumefikia mahali tulipo kutokana na wateja wetu kutuamini na kuendelea kutuunga mkono na ndio maana nasi tumeamua kutumia  kipindi hiki kuwasikiliza vilevile kuwasogezea huduma karibu na kwa mara nyingine napenda kusema Ahsante wateja wetu waliopo katika mtandao wetu na wale ambao hawajajiunga na mtandao wetu tunawakaribisha wajiunge ili waendelee kupata huduma bora”Alisema.
Ferrao alizitaja baadhi ya huduma za kampuni  hiyo ambazo zinaendelea kurahishisha maisha kuwa ni M-Mpesa ambayo inategemewa na makampuni na watu binafsi kutuma fedha na kufanya mihamala mbalimbali ya malipo kwa hapa nchini na ikiwa tayari imevuka mipaka ya nchi bila kusahau huduma ya Kilimo Klub ambayo imelenga kuwakwamua wakulima na kuwarahisisha maisha na huduma ya kutoa mikopo nafuu ya M-PAWA vilevile alitangaza kuzinduliwa kwa kifurushi kipya kinachojulikana kama Mpango mzima ambacho kinatoa unafuu kwa wateja kupata huduma za data.

Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo walisifu hatua ya Vodacom kuzindi kusogeza huduma karibu na wananchi “Huduma hizi zikisogea karibu nasi zinatupunguzia adha ya kutembea muda mrefu kuzifuata nawapongeza Vodacom kwa kuwajali wateja wake”.Alisema Abdulqadir  Rashid mmoja wa wateja aliyefika dukani hapo.

Tofauti na mwaka jana ambao kampuni  ya  Vodacom iliadhimisha wiki ya huduma kwa wafanyakazi wake kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii,mwaka huu wafanyakazi na maofisa wa kampuni wameweza kukutana na wateja na kuwaelimisha huduma mbalimbali za kampuni ikiwemo kusogeza huduma karibu kwa wateja kwa kufungua maduka sehemu mbalimbali jijini Dar es salaam na Masasi mkoani Mtwara. 

Katika mkoa wa dar es Salaam maduka ya Vodacom yamefunguliwa katika  sehemu za Ubungo,Mbezi Beach,Mbweni na kariakoo.Vodacom ina mtandao wa maduka ya kutoa huduma kwa wateja zaidi ya 100 kwa nchi nzima.
 Mbunge wa Ilala jijini Dar es Salaam,Musa Hassan Zungu(kulia)akisisitza jambo kwa Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(watatu toka kushoto)wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kutoa huduma mbalimbali za Vodacom Tanzania lililopo barabara ya uhuru kariakoo,wengine katika picha wa kwanza kushoto ni Ofisa mkuu wa mauzo na Usambazaji Keith Tukei na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.
 Mbunge wa Ilala jijini Dar es Salaam,Musa Hassan Zungu(kulia)akimsikiliza jambo Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(watatu toka kushoto)wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kutoa huduma mbalimbali za Vodacom Tanzania lililopo barabara ya uhuru kariakoo,wengine katika picha kushoto ni Ofisa mkuu wa mauzo na Usambazaji Keith Tukei na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.
  Mbunge wa Ilala jijini Dar es Salaam,Musa Hassan Zungu(katikati)pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) wakikata utepe kuzindua duka jipya la kutoa huduma mbalimbali za Vodacom Tanzania lililopo barabara ya uhuru kariakoo,wengine katika picha kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia na Mteja wa kwanza kufika katika duka hilo,Abdulqadir Rashidi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*