JPM AWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru pamoja na Dkt. Juma Mfinanga Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto Shukuru alikuwa akidaiwa kuishi kwa kula Sukari, Maziwa na mafuta ya kula lakini hali yake imeimarika zaidi na kuanza kula vyakula vya kawaida. Katikakati ni Mama yake Shukuru Mwanahabibi Mohamed Mtei.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Mujungu Museru mara baada ya kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika Wodi mbalimbali katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.