Magufuli asitisha usajili wa meli mpya Tanzania


"hatuwezi kucha jina la nchi yetu lichafuliwa na watu wanaofanya mambo kwa maslahi yao"- Rais wa Tanzania, John Magufuli
Image caption"hatuwezi kucha jina la nchi yetu lichafuliwa na watu wanaofanya mambo kwa maslahi yao"- Rais wa Tanzania, John Magufuli
Rais Magufuli amewaagiza Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi wa Tanzania pamoja na Waziri wa Ujenzi na Usafirishaji wa Zanzibar kusitisha usajili wa meli mpya nchini humo 'mpaka itakapotangazwa vinginevyo'.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, Rais wa Tanzania ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa meli zote 470 ambazo zimesajiliwa Tanzania na zinapeperusha bendera ya Tanzania.
Agizo hilo limekuja baada ya serikali ya Tanzania kufuta usajili wa meli mbili za kigeni wiki hii, baada ya taarifa ya kukamatwa kwa meli zilizokuwa zimepakia shehena za dawa za kulevya na silaha zikiwa zinapeperusha bendera ya Tanzania.
Miongoni mwa meli za kigeni zilizosajiliwa TanzaniaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMiongoni mwa meli za kigeni zilizosajiliwa Tanzania
"Fanyeni uchunguzi kwa meli zilizokamatwa ambazo ni 5 na pia hizi 470 zilizosajiliwa na zinazoendelea kufanya kazi zichunguzeni, hatuwezi kuacha jina la nchi yetu lichafuliwa na watu wanaofanya mambo kwa maslahi yao." amenukuliwa Rais Magufuli.
Serikali ya Tanzania imetangaza kuunda kamati ya pamoja ya wataalam bara na visiwani itakayoshirikisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kupitiwa upya usajili uliokwishafanyika na kuzihakiki taarifa za meli zote zilizosajiliwa nchini, kuangalia mwenendo mzima wa usajili, na hatimaye kutoa mapendekezo na ushauri kwa Serikali.
Aidha imebainika kuwa wenye meli hupendelea kusajili meli zao nje ya nchi zao kwa kukimbia uzito wa kodi na sheria zinazobana shughuli zao.

Mada zinazohusiana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA