NA MWANDISHI WETU, DAR BENKI ya NMB imeingia makubaliano rasmi (MoU) na Chama cha Wanawake Wamiliki wa Shule na Vyuo Tanzania (TAWOSCO), yaliyosainiwa sambamba na uzinduzi wa ‘NMB School Proposition, lengo likiwa ni kuwawezesha kupata mikopo yenye riba nafuu kwa maendeleo ya taasisi zao. MoU hiyo imesainiwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Bw. Juma Kimori na Katibu Mkuu wa TAWOSCO, Bi. Aisha Mzee, mbele ya Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng'i Issa, wakishuhudiwa pia na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi. Makubaliano hayo yanaleta sokoni Akaunti Maalum isiyo na Makato ya Mwezi kwa ajili ya kukusanya ada na michango mingine, Huduma ya Flex Malipo kuwezesha kukusanya malipo kupitia ‘Control Number’ na AdaBima ya kumwezesha mzazi anapopata ulemavu wa kudumu au kifo. Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Bw. Kimori alisema MoU hiyo itawezesha upatikanajiwa Huduma za Wakala, Lipa Mkononi (Lipa Namba na QR), p
- Get link
- Other Apps